Maskani

Invalid rotator ID specified (path erf_69_1370883686/erc_80_1370952142 doesn't exist). Unable to display rotator.
___________________________________________________________________
BARAZA KUU ni kifupi cha Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania. Ni chombo cha kiislamu kilichoundwa mwaka 1992 kwa madhumuni makubwa ya kuunganisha Jumuiya, Taasisi na Asasi za Kiislamu nchini Tanzania. Hii ni kutokana na mafundisho ya Quran kuwa:
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo  kumcha; wala msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili. Na shikamaneni kwa kamba (dini) ya Mwenyezi Mungu nyote ,  wala msiachane.” (3:102 – 103)
BARAZA KUU ni chombo kilichoundwa kwa nguvu ya Umma wa Kiislamu nchini. Nguvu hiyo ilitokana na kiu kubwa waliyonayo waislamu ya kutaka kujiletea maendeleo baada ya miongo mitatu (1961 – 1992)  ya Uhuru kupita bila ya mafanikio ya maana. Soma zaidi>>